Feature news

Fahamu faida na hasara za kurudiana na mpenzi wako wa zamani


NI IJUMAA nyingine tunapokutana jamvini! Shukrani za kipekee kwa Muumba wetu kwa kutuwezesha kuiona siku hii ya leo. Najua ni wengi walitamani kuiona lakini hawajafanikiwa. Nakukaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye jamvi letu tujadiliane na kuelimishana mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.

Bila shaka unawajua watu ambao walikuwa wakiishi pamoja kimapenzi, iwe ni ndoa, uchumba au uhusiano wa kawaida ambaowamewahi kutengana na baadaye wakarudiana, iwe ni mara moja au zaidi.

Yawezekana hata wewe ukawa miongoni mwa watu wa aina hiyo; kwamba uliwahi kutengana na mtu umpendaye lakini baadaye ukajikuta unarudiana naye na kuanzisha upya uhusiano. Je, kuna faida na madhara gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi unawachukuliaje?

NI JAMBO LA KAWAIDA KATIKA MAPENZI
Yawezekana aina hii ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya muda mkarudiana tena, likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi za Kiafrika lakini kwa taarifa yako, hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano wa kimapenzi duniani kote.

Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya wanandoa au watu ambao wapo kwenye uhusiano imara wa kimapenzi, wamewahi kupitia kipndi hiki kigumu cha kutengana na kurudiana, wengine wakifanya hivyo mara kadhaa.

Wapo baadhi ya watu ambao baada ya kutengana, hushindwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao hata kama bado wanapendana kwa kuona jamii itawashangaa kuwaona wakiwa pamoja tena baada ya kuachana kwa kashfa na vurugu kubwa. Kama na wewe ni miongoni mwa watu wa aina hii, narudia kukusisitiza kwamba hilo ni jambo la kawaida na linafanyika duniani kote.

MADHARA YAKE
Yapo madhara mengi yanayowakumba watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano. Inapotokea mmeachana na kila mmoja akaanzisha ukurasa mwingine wa mapenzi, lazima atakutana na mazingira tofauti kabisa na yale mliyozoea kuishi pamoja.

Endapo atakutana na mtu mwingine ambaye amekuzidi vitu vingi, hata ikitokea wakaachana na akarudi kwako, hawezi kukupenda kwa kiwango kile kama ilivyokuwa mwanzo kwa sababu tayari kuna vitu vipya vimeingia ndani ya kichwa chake na huo utakuwa ufa mwingine ambao siku za usoni utasababisha muachane tena.

Upo ushahidi wa wapenzi ambao baada ya kutengana na watu waliokuwa wanawapenda mwanzo, walikutana na watu wengine wenye uwezo wa kuwaridhisha na kuwafurahisha faragha kuliko ilivyokuwa kwenye uhusiano uliovunjika. Inapotokea ukarudiana na mpenzi wa aina hii, ambaye tayari ameshauona ulimwengu mwingine wa kuridhishwa kimapenzi ambao kwako hakuwahi kuuona, kamwe hawezi kutulia na wewe. Hesabu maumivu.

Suala jingine ni maradhi. Katika dunia iliyochafuka kama hii tunayoishi, ni hatari kurudiana na mwenzi wako kwa sababu hujui baada ya kutengana na wewe alikuwa akitoka na nani. Ni rahisi kukuletea maradhi ya zinaa au Ukimwi hasa kama alikuwa anatoka na watu wasio sahihi. Unapaswa kuwa makini katika hili.

Kulipizana visasi ni tatizo jingine linaloweza kuwakumba watu wanaoishi kwenye uhusiano wa aina hii. Yawezekana wewe ndiye uliyemuumiza mwenzi wako wakati mnaachana, ukautesa moyo wake na kushindwa kumuonea huruma wakati akiteseka. Inapotokea mmerudiana, wengi hubaki na vinyongo ndani ya mioyo yao na kwa sababu wewe ndiye uliyemuumiza, na yeye atakutafutia sababu ya kulipa kisasi ili na wewe uhisi maumivu kama aliyoyahisi yeye wakati mnaachana.

Hata hivyo, kama nilivyosema awali, suala hili siyo geni na linafanyika dunia nzima. Licha ya kueleza hasara zake, lazima zipo faida na ndiyo maana watu wanaendelea kuachana na kurudiana. Je, kuna faida gani kuishi katika uhusiano wa aina hiyo? Usikose kuungana nami wiki ijayo tuangalie faida zake.
Learn more »

Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio


Kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndo kila kitu.Ni kweli lakini kuwa na pesa bila wazo mahususi katika matumizi ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndo ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujisalisha. zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.

Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sababuni ya roho, mtonyo, mapene, ankara  na majina mengine mengi.  Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.
Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.

Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuana mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama ulikuwa hauna mapngo wa kununua kitu hicho. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha.

Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo lamsingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mapagalio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.

Kukopa pesa ovyo
Hili ndilo kosa kubwa ambao linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!  madeni yanavowatesa au yanavokutesa. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba.

Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja.  Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unanguna na wale wanaosema pesa ni shetani.

Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine hii itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa.

Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.
Learn more »

SABABU 7 ZA BAADHI YA WANAUME KUKIMBIWA NA WANAWAKE


Imezoeleka katika jamii kwamba wanaume hukimbiwa na wanawake kwa kukosa kipato au alichonacho ni kidogo, au muonekano na maumbile ya mwanaume bila kuzingatia kwamba wanawake huangalia vitu vingine zaidi ili kugundua kama wanaweza kuishi na aina hiyo ya mwanaume. Zifuatazo ni sababu 7 zinazowafanya wanawake wakimbie mahusiano na wanaume wenye tabia hizi:-

1.Kulazimishwa au kusukumwa kwenye maamuzi.

Wanawake hupenda mwanaume mwenye msimamo wake na mwenye kufanya maamuzi na kusaidia wenzie wanapohitahi msaada kutoka kwake pamoja nayeye mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa yeyote. Usisukumwe sukumwe hovyo hata kama ikiwa na mama yako hili huonyesha udhaifu.

2. Ulevi wa kupindukia.

Sawa, Unywaji wa pombe haujawahi kupingwa ila endapo mwanaume ni mnywaji kupindukia kiasi anaweza akalala hata baa, akaazisha ugomvi au kuzima kabisa haipendezi. Hakuna kitu wanawake wanachukia kama mwanaume asiwejiweza anapokunywa pombe.

3. Matusi na lugha chafu.

Inawezekana wote kuna wakati huwa tunajikuta tunatumia maneno makali kama matusi na lugha chafu lakini lakini sasa inapofikia 60% ya maneno yanayotoka mdomoni mwako ni machafu, tena bila hata kuzingatia mahali ulipo, haipendezi tena si kwa mwanamke tu. Wanawake huwafurahia wanaume wanaojua nini aseme na akiseme wapi. Lugha chafu na matusi hayatakufikisha popote kwenye sekta hii ya mapenzi.

4.Kulalamika kuhusu mpenzi wako wa zamani.
Hamna anayejali kwamba mpenzi wako alikua mdanganyifu, alikuchuna au Malaya, kumlalamikia mwanamke wako wa sasa kuhusu mwanamke mwingine kunazidi kukupunguzia nafasi yaw ewe kuwa na mwanamke wa sasa kwa muda mrefu 1) atafikiri licha ya yote, bado unampenda 2) atafikiri hicho ndicho utakifanya kwa anayefuata baada yake kwa maana kwa sasa unalalamika bila upande wa pili kuwepo hivyo waweza kuwa unadanganya na ndicho utafanya na baada ya mahusiano haya.

5.Mwanaume king’anganizi mwenye kuhitaji zaidi na zaidi. (Demanding)
Mwanaume analazimisha kupigiwa simu kila baada ya lisaa katika siku? Utadhani isipokua hivyo atafariki, na ukumbuke hapo hata hajawa Boyfriend bado, ndio kwanza anaongea na msichana. Jaribu kutafuta cha kufanya uwe busy kidogo hamna kitu kinakera kama mwanaume ambaye wanawake watafikiri hana kingine cha kufanya zaidi ya kufikiria mwanamke au mapenzi, mpe muda wa kukumiss ili akuze hisia zake kwako inavyotakiwa.

6.Mtu asiyeja familia wala rafiki zake.
Haitajalisha kabisa hata kama utamfanya yeye ajisikia kama Malkia, kama hujali familia yako hatavutiwa na wewe kwa imani kwamba utamfanyia hivyo nay eye pindi atakapokua mmoja kati ya wanafamilia kama mtafikia hatua ya kuoana. Jitahidi sana uwe na mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka, wanawake huliangalia hilo kwa wakati.

7. Uongo.

Kusema kweli, uongo kwa wanaume umekithiri, wengi wao huongea na uongo ili wapate wanachotaka vile inaaminika kwao bila longo longo maisha ya siku hizi huwezi kumpata mwanamke, la hasha, endapo mwanamke anagundua umemdanganya kitu, hata kama kilikua kidogo namna gani, imani na wewe inapotea. Hamna uongo mdogo na mkubwa, uongo ni uongo. Na hakuja jinsi ya kujielezea kwanini mtu ulidanganya wakati fulani na sasa unaamua kusema ukweli. Kuwa mkweli wakati wote.
Learn more »

Ebitoke Aondoka Timamu TV, Afuta Kila Kitu

Msanii wa maigizo ya vichekesho, Anastasia Exavery maarufu kama Ebitoke ambaye amekuwa akifanya kazi Timamu TV ametangaza kuondoka kuifanyia kazi TV hiyo mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Ebitoke amesema hayo kupitia ukurasa wake wa instagram na kudai kuwa kwa sasa atakuwa anafanya kazi na TV nyingine.

”Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu mashabiki na watu wote wanaonitazama na kusoma ujumbe huu, Kuanzia sasa nitakuwa nikifanya kazi zangu nje ya Timamu TV nikimaanisha mkataba wangu na Timamu TV umeisha” ameandika Ebitoke.

Nicki Minaj amwaga machozi akieleza alivyonyanyaswa na wapenzi
Aidha ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi mzima wa Timamu TV kwa kushirikiana pamoja katika kuhakikisha wanafanya kazi nzuri, lakini pia amewashukuru wafanyakazi wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao katika kutengeneza maigizo mafupi ya vichekesho ambao ni @ Bwanamjeshi na @Mr. Beneficial.

Ali Kiba afuta video ya wimbo wake mpya ‘Hela’, kisa…
Mbali na hatua hiyo  Ebitoke ameenda mbali zaidi kwa kufuta video zake zote za kazi alizofanya akiwa chini ya uongozi wa Timamu TV kwenye ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi Milioni 1.

Aidha hajasema baada ya kumaliza mkataba wake na Timamu TV atasajiliwa na TV gani nyingine kuendeleza fani yake ya uchekeshaji.
Learn more »

Rafiki Yangu Kanivuruga Akili Mnooo Kumuoa Msichana Aliyekuwa Mpenzi Wangu


Anajua Kabisa Yule Alikuwa Shemeji... Tena Hata Kesi Ndogo Ndogo Zilizotuhusu, Niliziweka Wazi Kwake Kwa Ushauri Na Msaada Wa Mawazo

Hata Tuliposhindwana Na Huyu Binti!.... Nilimshirikisha ......Na Kwakuwa Nilishavumilia Na Kuchoka Juu Ya Vitimbi Nilivyoangushiwa Na Huyu Binti, Akaafikiana Nami Kuwa Niachane Naye

Baada Ya Miezi Kadhaa......Cha Ajabu Kinachonishangaza Katika Hii Dunia Ni kupata Habari kuwa rafiki yangu yupo katika maandalizi ya kuoa na Mchumba wake ni yule yule aliyekuwa mchumba wangu siku za nyumba niliyeachana nae..Ki ukweli nimechanganyikiwa napata maswali mengi sana

Je inawezekana walikuwa wapenzi toka zamani ?
Je Rafiki yangu alihusika katika Kuvunja uchumba wetu ili yeye ajichukulie?

Nifanyaje Waungwana?
Learn more »

Njia Bora Kuliko zote ya Kuzuia Mimba Kwa Uzazi wa Mpangoa Kwa Wanawake Hii Hapa....



Elimu ya uzazi wa mpango bado haijawafikia vijana wengi sana hasa tanzania, wengi wao hudhani labda.

matumizi ya dawa na njia za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya malaya, watu waliokwisha zaa na kadhalika. lakini hii sio kweli kwani njia hizi ni nzuri kwa rika zote yaani vijana na watu wazima ambao wanashiriki ngono ila kwa sasa hawako tayari kupata mtoto.

kutotumika kwa njia hizi kumesababishwa kuzaliwa kwa watoto wengi ambao hawakupangwa, kujiua kwa wasichana kwa kukwepa aibu na utoaji wa mimba wa mara kwa mara.

utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba msichana akiingia kwenye mahusiano kwa miaka mitatu bila kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango anaweza kutoa mimba nne mpaka tano lakini pia asilimia kubwa ya wanachuo wa tanzania ambao huingia kwenye mahusiano vyuoni hawawezi kumaliza chuo bila kutoa mimba hata moja.

kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ikiwemo vitanzi, vijiti, kondomu,kutumia kalenda, sindano,vidonge, upasuaji wa kufunga mirija na kadhalika. kondomu ni njia bora sana kwani huzuia ukimwi na mimba pia lakini ukweli ni kwmba kama kondomu zingekua zinatumika vizuri basi hao watoto tusingewaona mtaani hivyo kama wewe hauko tayari kuzaa sasa hivi kwa sababu yeyote ile nakushauri utumie njia ya kijiti.

Njia hii ikoje?
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.

kwanini njia hii ni bora kuliko zote?
1. Hurudisha uwezo wa kuzaa haraka: kama unatumia kijiti hata kama kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata mtoto.

2. Ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.

3. Inafanya kazi kwa muda mrefu sana; kama wewe ni binti mdogo au wewe ni mama ambaye una mtoto tayari na hauhitaji mtoto kwa sasa njia hii ni nzuri kuliko zote kwani huweza kuzuia mimba kwa miaka mitano mfululizo kwa asilimia mia.

4. Haiingilii utoaji wa maziwa ya mama; vidonge vya uzazi wa mpango vyenye homoni zote mbili yaani oestrogen na progesterone kitaalamu kama microgynon huweza kupunguza wingi wa maziwa kwani wingi wake kwenye mfumo wa binadamu husababisha kupungua kwa homoni ya maziwa kitaalamu kama prolactin hormone.

5. Haiongezi uzito; inaaminika vidonge vya uzazi wa mpango huongeza uzito kwa kuzuia kiasi kikubwa cha maji kisitoke ndani ya mwili kwa njia ya mkojo na pia kuongeza hamu ya kula, lakini utafiti kwa wanaotumia vijiti haujaonyesha madhara haya.

6. Muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa hivyo ukitumia kijiti utapata faida hii.damu inaweza ikatoka hata mara mbili kwa mwaka tu.

7. Sio rahisi kwa watu wengine kujua: wasichana wengi hasa vijana hawapendi maisha yao ya ngono yafahamike, na hasa njia hizi za uzazi wa mpango watu wakijua unatumia wanakuona muhuni, kitu ambacho sio kweli, hivyo matumizi ya kijiti ni siri sana na sio rahisi kwa watu wengine kujua tofauti na vidonge ambavyo sio rahisi kuvificha.

Mwisho; utafiti unaonyesha utoaji wa mimba umewanyima wanawake wengi watoto, msanii maarufu wema sepetu ambaye kwa sasa anatafuta mtoto kwa shida sana aliwahi kukiri kwamba aliwahi kutoa mimba zamani kidogo na huenda anajutia maamuzi yake.hivyo kama wewe ni msichana mdogo na hutaki kuzaa kwa sasa au wewe ni mama hutaki mtoto mwingine kwa sasa tumia njia hii ya uzazi wa mpango itakusaidia sana


Learn more »

Wanawake, Hivi Mnajua Mwanaume Anayekutaka Kimapenzi au Anayekutamani?


Hii sasa ni kwa wanawake. Hivi mnajua mwanaume anayekutaka kimapenzi au anayekutamani jinsi anavyouangalia mwili wako anawasilisha hisia zake juu yako.

Je unawezaje kujua ujumbe anaokupa?

Mwanamke kama mwanaume anakutongoza na wakati unaongea naye yuko macho kodo kwenye matiti yako hapo jua kwamba akili yake imelenga zaidi sex hakuna mapenzi hapo yaweza kuwa one night stand, ukimpa humuoni tena.

Kama mwanaume uko naye kwenye mtoko na wakati anakutongoza anaangalia midomo yako kwa matamanio jua huyo yuko romantic kweli kweli na ana hisia za mapenzi juu yako. Huyu mnaweza kudumu kwenye mapenzi na hata kuoana kama ataridhishwa na tabia zako katika maeneo mengine.

Kama mwanaume anakuangalia machoni sana wakati wa mazungumzo yenu, basi hapo jua mwanaume anakuchunguza kama uko vizuri kiasi flani upstairs. Yaani anataka mwanamke smart kichwani na mwenye elimu nzuri kwahiyo kama na wewe uko vizuri kichwani jiuze hapo toa maujanja ma maujuzi uliyonayo ili kumvutia zaidi kama na wewe umempenda.

Yaani hapo hajali kuhusu mwili wako kwahiyo usipoteze muda mwingi kujiremba ukiwa na miadi naye wakati mwingine wewe noa akili yako tu umemaliza.

Ukiona mwanaume wakati anakutongoza anakuangalia zaidi mikono yako na mabegani huyo huwa anapenda vibaya yaani anapenda kumiliki na huenda wakati unakutana naye hajakutana kimwili na mwanamke kwa muda mrefu, kwahiyo hapo ujue kwamba mkikutana kimwili shughuli yake yaani mtoto hatumwi dukani.

Ukiona mwanaume anakutongoza lakini macho yake yako shingoni kodo kodo kuwa makini huyo ndiyo wale huanza kumpiga au kumfanyia mwanamke vitendo vya kikatili kabla au wakati wa sex. Hujulikana kama sadistic.

Ni watu ambao kwenye tendo la ndoa huwa kama vichaa na hufurahia na kulifurahia tendo la kujamiiana kwa kuona mwanamke aliye naye ameumia na hata kutokwa na damu.Wakati mwingine mchezo huo ukienda vibaya mwanamke huweza kupoteza maisha.

Lakini pia tatizo likiwa kubwa kuna wakati hufurahia kuua kati ya wanawake anakutaka nao kimwili na hiyo hutokea katika vipindi maalum.

Ukiona mwanaume anakutongoza lakini anakuangalia zaidi kiunoni au hips zako huyo anatarajia umzalie watoto.

Yaani huyo akikuoa utazalishwa wewe mpaka utengeneze timu ya mpira lakini wanajali familia.

Ukiona mwanaume anakutongoza lakini anaangalia zaidi miguu yako, huyo anakutaka ili ku show off kwa washkaji zake tu lakini siyo kwa lengo la kuwa na serious relationship.

Hapo unakuwa wa kuchezewa tu......

Learn more »

Banner1

Banner1