SABABU 7 ZA BAADHI YA WANAUME KUKIMBIWA NA WANAWAKE
Imezoeleka katika jamii kwamba wanaume hukimbiwa na wanawake kwa kukosa
kipato au alichonacho ni kidogo, au muonekano na maumbile ya mwanaume
bila kuzingatia kwamba wanawake huangalia vitu vingine zaidi ili
kugundua kama wanaweza kuishi na aina hiyo ya mwanaume. Zifuatazo ni
sababu 7 zinazowafanya wanawake wakimbie mahusiano na wanaume wenye
tabia hizi:-
1.Kulazimishwa au kusukumwa kwenye maamuzi.
Wanawake hupenda mwanaume mwenye msimamo wake na mwenye kufanya maamuzi
na kusaidia wenzie wanapohitahi msaada kutoka kwake pamoja nayeye
mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa yeyote. Usisukumwe sukumwe hovyo hata
kama ikiwa na mama yako hili huonyesha udhaifu.
2. Ulevi wa kupindukia.
Sawa, Unywaji wa pombe haujawahi kupingwa ila endapo mwanaume ni mnywaji
kupindukia kiasi anaweza akalala hata baa, akaazisha ugomvi au kuzima
kabisa haipendezi. Hakuna kitu wanawake wanachukia kama mwanaume
asiwejiweza anapokunywa pombe.
3. Matusi na lugha chafu.
Inawezekana wote kuna wakati huwa tunajikuta tunatumia maneno makali
kama matusi na lugha chafu lakini lakini sasa inapofikia 60% ya maneno
yanayotoka mdomoni mwako ni machafu, tena bila hata kuzingatia mahali
ulipo, haipendezi tena si kwa mwanamke tu. Wanawake huwafurahia wanaume
wanaojua nini aseme na akiseme wapi. Lugha chafu na matusi
hayatakufikisha popote kwenye sekta hii ya mapenzi.
4.Kulalamika kuhusu mpenzi wako wa zamani.
Hamna anayejali kwamba mpenzi wako alikua mdanganyifu, alikuchuna au
Malaya, kumlalamikia mwanamke wako wa sasa kuhusu mwanamke mwingine
kunazidi kukupunguzia nafasi yaw ewe kuwa na mwanamke wa sasa kwa muda
mrefu 1) atafikiri licha ya yote, bado unampenda 2) atafikiri hicho
ndicho utakifanya kwa anayefuata baada yake kwa maana kwa sasa
unalalamika bila upande wa pili kuwepo hivyo waweza kuwa unadanganya na
ndicho utafanya na baada ya mahusiano haya.
5.Mwanaume king’anganizi mwenye kuhitaji zaidi na zaidi. (Demanding)
Mwanaume analazimisha kupigiwa simu kila baada ya lisaa katika siku?
Utadhani isipokua hivyo atafariki, na ukumbuke hapo hata hajawa
Boyfriend bado, ndio kwanza anaongea na msichana. Jaribu kutafuta cha
kufanya uwe busy kidogo hamna kitu kinakera kama mwanaume ambaye
wanawake watafikiri hana kingine cha kufanya zaidi ya kufikiria mwanamke
au mapenzi, mpe muda wa kukumiss ili akuze hisia zake kwako
inavyotakiwa.
6.Mtu asiyeja familia wala rafiki zake.
Haitajalisha kabisa hata kama utamfanya yeye ajisikia kama Malkia, kama
hujali familia yako hatavutiwa na wewe kwa imani kwamba utamfanyia hivyo
nay eye pindi atakapokua mmoja kati ya wanafamilia kama mtafikia hatua
ya kuoana. Jitahidi sana uwe na mahusiano mazuri na watu wanaokuzunguka,
wanawake huliangalia hilo kwa wakati.
7. Uongo.
Kusema kweli, uongo kwa wanaume umekithiri, wengi wao huongea na uongo
ili wapate wanachotaka vile inaaminika kwao bila longo longo maisha ya
siku hizi huwezi kumpata mwanamke, la hasha, endapo mwanamke anagundua
umemdanganya kitu, hata kama kilikua kidogo namna gani, imani na wewe
inapotea. Hamna uongo mdogo na mkubwa, uongo ni uongo. Na hakuja jinsi
ya kujielezea kwanini mtu ulidanganya wakati fulani na sasa unaamua
kusema ukweli. Kuwa mkweli wakati wote.
0 comments: