Ushuhuda: Wazazi Wanalinda Watoto Dhidi ya Watu wa nje Wakati Waharibifu Wako Ndani ya Familia

Mimi nimekulia mazingira ya kuchungwa sana. Nilikuwa siruhusiwi hata kujichanganya na watoto wenzangu zaidi ya wa shuleni tu. Hata kukiwa na birthday ya rafiki yangu wazazi hasa mama hakuwa akiniruhusu. Alikuwa anadhani sijui nitaharibika au sijui alikuwa kwanini anafanya hivyo.

Sasa kuna kipindi mtoto wa mama yangu mdogo alikuja kukaa nyumbani. Alikuwa amemaliza form six anasubiria majibu. Kwa wakati huo kulikuwa hakuna dada wa kazi.

Tukirudi shule baada ya kula kawaida wote tunalala lakini akawa anawaambia wadogo zangu wao wasilale waende wacheze nje halafu mimi ndio naambiwa nilale. Kwa njia hiyo akanifanyia anachotaka kunifanyia.

Nakumbuka sikuweza kwenda shule takribani wiki nzima. Niliumww nikapelekwa hospitali nikapatwa na malaria na dawa nilimeza. Sikuwahi kuwaambia wazazi wangu, akaendelea na tabia yake hiyo mpaka akaja kuondoka.

Mara nyingine mtoto wa aunt yangu alinifanyia kitendo kinachofanana na hiko. Kipindi hiko sisi na aunt yetu tulikuwa tunaishi karibu. Sisi Tabata Bima aunt yangu anaishi Tabata Alfaruk; sio mbali ziko karibu karibu.

Nilikuwa standard 7 yeye mtoto wa aunt yangu ambae ni kaka yangu alikuwa anasoma chuo sijui IFM sikumbuki vizuri. Mama akaniambia niwe naenda ananifundisha mathematics nilikuwa naenda Ijumaa hadi Jumapili.

Huyu kaka yangu ambae mtoto wa aunt yangu pia akanifanyia anachotaka kunifanyia. Kuna siku aunt yangu alitukuta tukiwa pamoja alimgombeza mtoto wake akampiga lakini akanibembeleza nisije kumwambia baba na mama au mtu mwingne.

Yote yanatokea sikuwahi kumwambia mtu yoyote zaidi ya leo naandika hapa. Lakini kitu ambacho najiuliza kwanini wazazi wangu walijitajidi sana kunizuia na watu wa nje ya nyumbani wakasahau kunizuia na watu wa karibu yangu mpaka nikawahi kufanyiwa mambo ya utuuzima nikiwa na miaka kumi tu.

Natamani siku niwaulize kwanini waliwaamini sana watu juu yetu sisi lakini siwezi sababu hawajui sikuwaambia na sitawaambia itabaki siri yangu. Lakini siku hata nikawa na familia yangu siwezi kuamini mtu yoyote juu ya watoto wangu

Hili ni funzo sana kwangu!

0 comments:

Banner1

Banner1