Mwanamke Hupaswi Kutoa siri za Chumbani kwa Rafiki zako
Shoga yangu, kama ilivyo ada, ni Jumatatu nyingine ambapo tunakutana katika safu yetu hii kwa ajili ya kuelimishana na kukosoana mambo mbalimbali hususan ya mapenzi. Basi leo shoga yangu nataka kuzungumza nawe kuhusu tabia ya baadhi ya wenzetu kuzungumza siri za waume zao saluni au wanapokuwa wameketi na shoga zao mahali fulani.
Shoga, hakuna kitu ambacho mwishoni huleta kilio kwa mwanamke kama kutoa siri za mumewe nje kwa sababu mwanaume ambaye huenda hayuko vizuri awapo kwenye uwanja wa fundi seremala akigundua mkewe ndiye kaivujisha siri hiyo kwa wenzake hapo kitakachofuata ni talaka tu!
Siyo siri hiyo tu, hata kama katimuliwa kazini na maisha yake kumwendea kombo, akijua mkewe anapita kila mtaa akiwaambia shoga zake jambo hilo, mumewe akijua kitanuka tu!
Athari zingine za kutoa siri hizo ni pale mwanamke anapofikishwa vizuri sehemu anayoitaka na mumewe, kwa kujiona anafaidi akiwaambia shoga zake namna anavyofurahia chakula cha usiku ni wazi nao watapenda kukionja chakula hicho.
Shoga zake hao, watafanya kila wawezavyo kumtega mumewe na akishaingia kwenye anga zao wataongeza manjonjo na jamaa akinogewa atapiga kambi ya kudumu kwa shoga yako kisa ni wewe kutoa siri za ndani nje.
Hivi shoga yangu, kuna haja gani ya kuwaambia wenzako kwamba mumeo akikushika mnapokuwa chumbani lazima akutoe machozi? Hujui kama nao watatamani watolewe machozi?
Kumbuka kwamba karne hii kuna tatizo la wanaume kutojiweza kwenye makasheshe hivyo wanawake wengi hubaki na kiu zao sasa utakapowaambia jinsi wewe unavyofurahia kugaragazwa na mumeo, utasababisha wawe na hamu na kitakachofuata lazima wakuibie penzi lako kwa gharama yoyote.
Shoga, jiepushe sana na tabia ya kuwaambia wenzako mambo ya ndani yakuhuyo wewe na mumeo kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa ndoa yenu na maisha ya mumeo pia. Bye!
0 comments: