Kisa Cha Mama Mkwe Wa Mwendo Kasi
“Mpaka sasa hivi bado anaendelea kukupiga?” Mama John alimuuliza
mkwe wake.” Ndiyo mama tena amezidi, yaani kila siku nimekuwa kama
ngoma, nimechoka Mama nibora nirudi kwetu, kwetu sijaua Mama..” Anna
alaiongea huku akitokwa na machaozi. Mama mkwe wake alimuangalia kwa
huruma, kisha akamuambia.
“Usiondoke mwanangu, nitaongea naye…”
“Haitasaidia chochote Mama, mara ngapi tumekaa vikao kuongea naye
lakini habadiliki. Wanangu wameshakuwa wakubwa naondoka, sitaki
kuendelea kuteseka…”
“Hapana usiondoke mwanangu, sasa hivi nilazima akusikilize…”. Anna
alikuwa amekata tama, miaka nane ya ndoa yake ilikuwa ya mateso sana na
mara kadhaa alishamlalamikia mama mkwe wake kuhusu tabia ya mumewe
kumpiga lakini haikusaidia.
Kila mara mumewe alisema atajirekebisha anapokuwa mbele ya wazazi
wake lakini akifika nyumbani huanza upya akimpiga hata kwa kushitaki.
Anna alishafanya mamauzi ya kuachana na mumewe, tayari alishapata chumba
chake na alienda kumpa tu taarifa Mama mkwe wake ambaye walikuwa
wakipatana sana.
“Wewe nenda nyumbani nitakuja huko huko kuongea naya, safari hii
atanisikiliza, si bado mnafuga Kuku?” Mama mkwe wake alimuuliza swali
ambalo hakuelewa kuwa lilikuwa linahusiana na nini na kupigwa kwake,
lakini alijibu. “Ndiyo Mama bado tunafuga…”
Alijibu na Mama mkwe wake alimuambia kwenda nyumbani kwake na kesho
yake angeenda kuwatembelea. Anna aliondoka akiwa na wasiwasi, wazo la
kumuacha mumewe lilikuwa palepale, hakuwaza ni kitu gani ambacho
angefanya ambacho kingemfanya kubadilisha mawazo yake.
*****
Jioni ya siku iliyofuata Mama John alifika nyumbani kwa mwanae,
John alikua bado hajatoka kazini na Anna alikuwa akijiandaa kupika
chakula cha usiku, Mama John alimuambia mkwe wake siku hiyo anataka
kupika yeye. Ingawa Anna hakutaka lakini alilazimishia mpaka akawa hana
namna, aliingia jikoni na kuanza kupika akiwaambia watu wote kukaa
sebuleni kuangalia TV.
John aliporejea alimkuta mkewe na watoto wakiangalia TV aliambiwa
Mama yake yupo na yuko jikoni anapika, alitaka kufoka kwanini mkewe
anamufanyisha kazi Mama yake ambaye alikuwa mzee lakini Mama yake
alitokea na kumuambia yeye ndiyo kaamua kupika.
John alikuwa ampole kwani pamoja na ukali wake kwa mkewe lakini
bado alimpenda na kumuogopa Mama yake kama mtoto. Alikaa kistaarabu
sebuleni kama mkewe, Mama yake alimaliza kupika na kutenga chakula
mezani, Anna na Mfanyakazi wa ndani walipotaka kumsaidia alikataa na
kusema atafanya kila kitu mwenyewe.
Alitenga chakula mezani na kumpakulia kila mtu kwenye sahani kisha
akawakaribisha. Ingawa haukua utaratibu kwa maana kila alikuwa akipakua
chakula chake mwenyewe lakini hakuna aliyeongea, wote walifurahia
chakula cha Mama.
Wakiwa wamekaa mezani baada ya sala, John alichukua kijiko na
kuchota chakula, alipandisha mkono wake kukiweka mdomoni lakini kabla
hajafika mdomoni Mama yake ambaye alikaa pembeni yake akimuangalia
alikipiga kile kijiko chakula kikamwagika.
“Acha kula hicho chakula, chukua hiki?” Mama John
aliongea huku akichukua sahani iliyokuwa na chakula cha John na
kumsogezea ile ya kwake. Watu wote walishangaa kwa kile kitendo lakini
Mama John hakujali, aliichukua ile sahani na kijiko alichotumia John
akarudi jikoni kisha baada ya muda akarudi na sahani nyingine ambayo
alikula yeye.
John aliuliza nini kinaendelea lakini Mama yake alifoka “Kula,
hakuna kuongea wakati unakula! Unakuwa kama sikukufundisha nidhamu?”
Mama yake alimjibu kwa sauti ya juu. Waliendelea kula kimya kimya,
hakuna aliyetaka kuongea.
*****
Baada ya kumaliza kula, Mama John hakutaka mtu aguse vyombo,
aliondoa vyombo mwenyewe na kuvipeleka jikoni. Kila kitu kilikuwa
chakushangaza hawakujua kwanini kaamua kufanya hivyo. Baada ya kuondoa
vyombo na watoto wenda kulala, ulikuwa ni wakati wa wakubwa nao kulala.
Kabla ya kwenda kulala Mama John alirudi jikoni na kuchukua sahani
ya chakula, ilikuwa ni ile ambayo alimkataza mwanae kula. “Naomba
mnisindikize nnje..” Aliwaambia na wao bila kujua kuwa alikua anataka
kufanya nini walinyanyuka na kuongozana naye, “Uje na funguo za banda la
Kuku”. Aliamrisha na Anna alienda kuchukua funguo la banda la Kuku.
Walifika katika banda la Kuku, kulikuwa na mabanda matatu, Mama
John aliwaambia kufungua moja ambapo alimwaga kile chakula kwenye lile
banda la Kuku ambao walianza kukimbizana, alifunga banda na kuwaambia
waende wakalale. Bila kujua sababu zake za kufanya hivyo waliingia ndani
kulala kila mmoja akiwa na mawazo yake.
*****
Siku iliyofuata ilikua ni Alhamisi hivyo Anna na Mumewe walitakiwa
kwenda kazini. Waliamka mapema na kukuta Mama mkwe kashaamka zamani na
kashaandaa chai, ulikua ni mshangao kwani mara kadhaa alikuja kukaa pale
na hakuwa akifanya hivyo. Aliwaandalia chai mezani na kwa mara nyingine
John alipotaka kunywa alimzuia na kubadilisha kikombe.
Walimuuliza kwnaini anafanya hivyo lakini alikataa kuwajibu
akiwaambia wanywe chai kwanza. Walikunywa chai na baada ya kumaliza
wakati wakitaka kuondoka, aliwaambia waende kwanza kwenye banda la Kuku.
Walifika na baada ya kuangalia, katika mabanda mawili hakukuwa na kitu,
Kuku walikuwa salama.
Lakini katika banda lile ambalo alikua wamemwagia chakula ambalo
lilikua na kuku zaidi ya kumi, wote walikuwa wamelala chini wamekufa.
John na mkewe walistuka na kushangaa nini kimetokea, Mama yake
aliwaangalia akiwa maetulia kwa muda kisha akasema.
“Unaona mwanangu, hicho ndiyo chakula nilichokutengea mezani jana.
Nilikuwa nimeweka sumu kama ambavyo nimeweka katika chai asubuhi, kijiko
kimoja tu au funda moja la chai vilitosha kukufanya kuwa kama hao Kuku
hapo!” Aliongea huku akiwaangalia namna walivyokuwa wanashangaa midomo
mizito hata kufunguka.
“Jana niliokoa maisha yako, lakini ningeweza kukuacha ule na subuhi
ukaamka kama hao Kuku nikawaambia majirani umekufa kwa presha kama
ambavyo naweza sema hawa Kuku wamekufa na kideri…
Mkeo kila siku analalamika unampiga, kila siku nakusihi acha
kumpiga mkeo lakini husikii. Jana alikuja kwangu na kuniambia kuwa
kachoka na anataka kuondoka, huyu ni mke mwema, wengine wanapochoka
hawaondoki bali wanakuondoa wewe.
Nikuulize kitu kimoja wakati una miaka mingapi?” John alilisikia
swali lakini hakuweza hata kujibu bado alikuwa ameshikwa na butwaa.
“Huwezi kujibueee… mimi nakumbuka miaka 35, hembu niambie wakati unakua
kuna Babu yako hata mmoja ambaye ulimuona…?
“Hapana, hata siwakumbuki…” John alijibu kinyonge kabisa.
“Na Bibi zako…”
“Wote wapo mpaka sasa…”
“Nadhani sasa umepata jibu… chezea kila kitu lakini si
mwanamke anayekupikia chakula! Usifikiri kila mwanaume anayekufa ni
Mungu kapanga, wengine ni wake zao wamechoka tu kupigwa na kunyanyasika.
Mke wako anaondoka kwakuwa ana kazi anajua anaweza kujihudumia, hembu
jiulize kama angechoka halafu hana kazi anajua ukimuacha anaenda kuwa
ombaomba…
Mimi ni Mama yako nimeona mengi, acha kujifanya mwanaume kuliko
wanaume wengine, mwanaume kamili hampigi mke wake anenda kupigana na
wanaume wenzake. Mimi naondoka, sitegemei kusikia umempiga mkeo tena…
Kama unataka kuendelea kumpiga basi anza kupika mwenye…” Mama John
alimaliza kuongea kisha akarudi ndani akiwaacha wote wameduwaa,
alichukua mfuko wake aliokuja nao na kutoka nnje kuondoka. Alirudi na
kumuona mwanaea amepiga magoti akimuomba mkewe msamaha…”
Anna alikubalia kumsamehe mume wake ambaye aliahidi kutokurudia
tena. John aliahidi kubadilika na kweli alibadilika, alianza kuwahi
kurejea nyumbani na kurudisha mapenzi yote kama kipindi cha uchumba,
hakumpiga tena mkewe na sasa ndoa yao ina miaka kumi na tano bila ugomvi
wowote.
****MWISHO****
0 comments: