FANYA Yoote Ufanyayo..Lakini Mwisho Unapaswa Ujue Je Mpenzi Wako Amekuweka Katika Kundi Gani Kati ya Haya Matatu?
KATIKA mapenzi kuna mambo mengine yanaumiza, lakini ni vizuri kujifunza. Ukijua inakuwa rahisi kukaa nayo mbali.
Kuna kitu nataka kukupa rafiki yangu mpendwa. Je, unajua kuwa baadhi ya wanawake huwaweka wanaume katika makundi?
Ndugu zangu baadhi ya wanawake wasio waaminifu wenye wanaume zaidi ya Mmoja, huwaweka wanaume kwenye makundi matatu.
Unaweza
kuwa na msichana mkapendana sana, kwa sababu ya upofu wa mapenzi usijue
amekuweka kundi lipi. Ni vizuri kuyafahamu makundi hayo kisha
kujichunguza ili ujue kundi ulilopo.
MAKUNDI
Makundi hayo ni starehe, kutoshelezwa kimapenzi na fedha. Lazima uwe makini sana ili uweze kujua tabia za makundi hayo.
Inahitajika
utulivu na umakini wa hali ya juu maana wakati mwingine mwanamke
anaweza kuonyesha dalili ya wazi ya kundi Fulani, lakini kutokana na
kupumbazwa na mapenzi ukaamini kwamba umefika kwenye kiota cha raha za
wapendanao.
KUNDI A
Unaweza
kuwa kwenye kundi la starehe. Mwanamke akawa na wewe kwa lengo la kuwa
na uhakika wa kupata starehe kila wiki. Hebu angalia tabia za mpenzi
wako, yukoje?
Haina
maana kwamba mwanamke akipenda starehe ni tatizo, lakini ukiona
mazungumzo yake yanaonekana kujali zaidi starehe kuliko mambo mengine
muhimu, ujue hapo upo kwenye mikono isiyo salama.
Mwanamke mwenye upendo wa dhati hawezi kuendekeza starehe, sana sana atakusubiri umshinikize mtoke.
KUNDI B
Wapo wanawake ambao wapo na wanaume kwa ajili ya kujipatia fedha.
Fikra
zao zote ni kupata fedha na si kitu kingine chochote. Atafanya kila
kitu, atatafuta kila sababu lakini lengo lake ni kukuchuma.
Wanawake
hawa wapo wa aina mbili, wengine huchuna fedha na kwenda kula raha na
wanaume wengine, huku wengine wakiwa ni wachumi kwa manufaa yao wenyewe.
Wachumi
mara nyingi huwa na wanaume wengi wakiwa na lengo la kujipatia fedha.
Ni kama wanajiuza lakini hawapo sokoni rasmi. Mwanamke wako yukoje?
KUNDI C
Kundi
la mwisho ni lile la wanawake wanaotaka wanaume wa kuwatumia kimapenzi
tu. Huyu hata usipompa fedha, shida yake kubwa huwa ni faragha.
Mara
nyingi mwanamke wa aina hii anaweza kuwa mkubwa kiumri kuliko mwanaume
lakini wakati mwingine anaweza kuwa na umri wa kati, sawa au chini ya
mwanamume, lakini haonyeshi nia ya malengo ya ndoa siku zijazo.
Huyu
ni rahisi kumgundua hata katika mawasiliano tu. Anaweza kukuambia
waziwazi anakutaka faragha, tena mara kwa mara. Hazungumzii maendeleo,
hataki kujua habari zako, anachotaka ni mapenzi tu.
Asilimia
kubwa ya wanawake wa namna hii ni wale ambao wana wenzi wengine wenye
malengo nao lakini hawawatimizii haja zao za kimapenzi.
0 comments: