Mwongozo Utakaokusaidia Kuondokana na Mawazo Mabaya


Mbinu Itakayokusaidia kutambua na kubadili mawazo  mabaya yanayokuja kwako mara kwa mara .
fotolia_86800014_s-144x144-315_0-504_503 Mwongozo Utakaokusaidia Kuondokana na Mawazo Mabaya
Tamaa mbaya, mawazo mabaya, mitazamo mibaya  inayotokea kwenye maisha yako yanaweza kutoweka kwa urahisi kuliko unavyofikiria . Unapokuwa unafikiria vibaya kila mara unaongeza  risk ya uharibifu wa akili yako,  unasababisha matatizo ya afya yako, Mahusiano yako, kipato chako hakiwezi kukaa vizuri.
Lakini habari ya mijini ni hii , kila mtu anaweza kujifunza jinsi ya kuondokana na Negative thinking. Mimi nimejifunza kitu kikubwa hapa, Kwamba mtu anapoamua kujifunza  kubadilisha mawazo mabaya aliyonayo juu ya kitu chochote , sio tu atajisikia vizuri bali  tabia inabadilika pia.
Kutengeneza tabia nzuri ni ngumu , lakini kuishi tabia nzuri ni rahisi. Na kutengeneza tabia mbaya ni rahisi lakini kuishi tabia mbaya ni ngumu kupita kiasi.  Wazazi wengi wanalea watoto kimayai , wanasahau kuwa kiburi cha mtoto kinaanzia akiwa na umri wa miaka 3. Hapo usimnyime mtoto fimbo kila anapokosea. Ni vizuri kuanza kujenga misuli ya akili inayofikiri mazuri mapema.
Jinsi Gani Unaweza Kubadilisha Mawazo Mabaya.
Mawazo haya husimamia  hapa;  Kujilaumu, kutazama Habari mbaya, Huzuni ya kuotea, mawazo mabaya juu ya wengine, kazi , biashara, mahusiano.   Usipokuwa makini unaweza kufikiri ni mawazo mazuri lakini sio.  Tambua ni jinsi gani  mawazo mabaya yanavyokuja kwako.
1.Kujilaumu. Mahali ambapo unatakiwa kuchukua jukumu lako  na kujiona kuwa huwezi kutimiza lengo kutokana na tatizo la kiakili  ndani yako ni kutokujua kutumia muda wako vizuri. Kila kitu utakuwa unaona kama unaharibu. Jaribu kutazama muda ulionao na ule ambao umetumia  unapokuwa unajilaumu utagundua kuwa  kuna tatizo ndani yako mwenyewe.
2.Kutazama Habari Mbaya;  Kama kuna mambo tisa mazuri  yametokea kwa siku,  Utaona jinsi  inavyokuwa rahisi kufuatilia lile moja baya badala ya kufuatilia mengi mazuri. Lakini tambua kuwa kuzamia kwenye mawazo hayo mabaya  yatakukwamisha kwenye giza kubwa na ukiwa na utupu mkubwa. Ni muhimu kurudi kwenye mazuri kila mara unapoona dalili hio mbaya. Rudi kwenye Nuru.
3.Huzuni Ya Kuotea. Hata kama hujui ni kitu gani kitatokea kesho,  Ni vizuri kjijengea tabia ya kuwaza mema kila mara. Muombe Mungu kila siku akujaze Tunda la roho ndani mwako. Neno la Mungu Linasema kuwa Katika Mathayo 7:7 Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, Bisheni nanyi mtafunguliwa. Kama unaona upungufu  wa kitu ndani yako muombe Mungu. Yakobo 1:5. mtu wa kwenu akipungukiwa na …. Na aombe Dua kwa Mungu awapaye wote kwa ukarimu.
Huenda unakuwa na wasiwasi wa kutokupandishwa cheo, kutokupata wateja,  kuharibika kwa mahusiano, kutokupona ugonjwa ulionao, Huzuni ya kuotea isikuharibie utabiri wako mzuri kwa ajili ya kesho yako.
4.Kujishusha Hadhi;  Kujisemea maneno mabaya mwenyewe, mfano umeenda kwenye usaili na kujiona kama  umefanya vibaya kabla ya matokeo au kujishawishi mwenyewe kuwa huwezi kupata kazi . Kwa jinsi unavyozidi kuwaza mabaya  ndivyo unavyojishusha chini zaidi. Na jinsi unavyojisikia vibaya  unashindwa kuwaza mazuri.
Kitu Gani Cha Kufanya Mara Unapoona Hali Hio Inakupata.
Mara tu unapotambua hali hio inakutokea . Haraka sana Angalia muda wako unatumiaje, Isije ikawa akili yako imekuwa karakana la Adui . Akili ikiwa bize huwezi kuwaza mabaya. Jiulize mwenyewe kama Unawafanyia watu kile ambacho unapenda wewe ufanyiwe? Ukiwa unajiwazia mabaya mwenyewe, utafungulia mlango wa watu kukuwazia mabaya pia. Jiulize kama ungeweza kusema nini kwa rafiki ambaye ana tatizo kama hilo?
Fanya mchakato mpya wa kusave pesa za kutosha kwa ajili ya baadae.
Thubutu leo kujisemea maneno mazuri , na ukumbuke kuwa kujenga tabia nzuri sio siku moja, kwa hio usikate tamaa, dhamiria kubadilika. Inawezekana.
Tambua kuwa kuwekeza inahitaji juhudi kubwa.  Kubadilika kimwili inategemea sana mabadiliko ya kiroho . Ubongo wako unakusubiri wewe kufanya maamuzi  ya kitu gani unataka katika maisha yako.
Subscribe  . kupata makala mpya.

0 comments:

Banner1

Banner1