Mke Wangu Ana Mimba, Katokea Kunichukia na Kampenda Mume wa Mtu Jirani na Chumba Tulichopanga
Mimi kijana mwenzenu nasikitika sana na hii tabia ya mke wangu, kwakweli ana nichanganya sana jamani
Ana mimba ya miezi sita lakini katokea kunichukia sana jamani hataki hata kunisogelea wala kula chakula mezan pamoja na mimi
Lakini katokea kumpenda mme wa mtu ambaye ni jirani wa chumba hapa tulipopanga
Mke wangu ni mama wa nyumban na hana kaz lakin mimi huondoka asubuh sana kwenda job lakin hurud usiku wa saa tatu
Nikifika nyumban get had nije nifunguliwe na mtu mwingine mke wangu yeye kalala tu na hata kama nikifika mlangon huwa hafungui upes yaan nitagonga mlango had bas na atakuja kufungua mda atakao taka yeye
Mfano jana nimefika nyumban saa tatu lakin alikuja kunifungulia saa tano usiku
Na kama nikiingia ndani anaanza kutema tema mate eti kuna kitu ndani kinanuka shombo ya samaki hasa mimi nikiingia
Yaani nakuwa naambiwa mda mwingine yule jamaa huwa anaingia hadi ndani mwangu kupiga story na mke wangu
Nateseka sana jaman
Naomben ushauri wenu
0 comments: